1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Itakuwa kosa Ufaransa kukataa katiba ya Ulaya

19 Aprili 2005

Ufaransa itakuwa imefanya kosa kubwa iwapo itaikataa katiba ya Umoja wa Ulaya lakini Ujerumani inataraji itaimarisha azma yake ya kuidhinisha katika bunge hapo mwezi ujao.

Waziri wa mambo ya ndani ya Ujerumani Otto Schily amesema katika hotuba mjini Berlin leo hii anatarajia sana kwamba kushawishiwa kwa wananchi wa Ufaransa kutafanikiwa na kwamba watakuwa wamefanya kosa kubwa iwapo kura hiyo ya maoni itashindwa.

Amesema hilo litakuwa pigo kubwa kwa sera ikiwemo ya mambo ya ndani ya nchi na sheria barani Ulaya.

Ujerumani haitokuwa na kura ya maoni lakini inapanga kuidhinisha katiba hiyo katika bunge hapo mwezi ujao kabla ya kura ya maoni ya Ufaransa iliopangwa kufanyika May 29.