BERLIN: Jung amelaani shambulizi la kujitolea muhanga
6 Oktoba 2007Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amelaani vikali shambulizi la kujitolea muhanga lililofanywa dhidi ya wanajeshi wa Ujerumani kaskazini mwa Afghanistan.
Siku ya Ijumaa,wanajeshi 3 wa Kijerumani na mkalimani wao wa Kiafghanistan walijeruhiwa katika shambulizi hilo,karibu na mji wa Kunduz.