BERLIN : Kampuni ya simu ya Ujerumani yashindwa kwenye ushindani
10 Agosti 2006Matangazo
Kampuni ya simu ya Ujerumani Deutsche Telekom imepugunza makadiriro yake ya mapato na mauzo kwa mwaka 2006 na 2007 na kulaumu ushindani mkali wa bei uliopo nchini Ujerumani.
Mapato ya kipindi cha theluthi ya pili ya mwaka ya kampuni hiyo ya simu kubwa kabisa barani Ulaya yameshuka kwa asilimia saba na ushee.Mauzo ya simu za mkono yameshindwa kuziba hasara wakati wateja wakikimbilia kwenye simu rahisi na huduma nafuu za mtandao.
Kampuni hiyo ya Telekom inatarajia mauzo yataongezeka kwa wastani hapo mwakani.