1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela Angela Merkel atoa wito kukabiliana na Manazi-mamboleo.

28 Januari 2007

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, ametoa wito wa kuwepo juhudi mpya kukabiliana na manazi mambo leo hasa chama cha mrengo wa kulia cha National Democratic Party, NDP.

Bibi Angela Merkel amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya ukumbusho wa mauaji ya wayahudi, hasa kuvunjwa kambi kubwa zaidi ya manazi ya Auschwitz mwaka alfu moja mia tisa na arubaini na tano.

Sherehe zimeendeshwa katika maeneo mengi ya Ujerumani kukumbuka siku hiyo.

Wakati huo huo rais wa bunge la Ulaya mjini Brussels, Hans-Gert Poettering amesema vitendo vya manazi ni lazima vikumbukwe ili iwe tahadhari ya kuzuia kuzuka mauaji mengine ya halaiki kama hayo siku za usoni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW