BERLIN: Kansela Gerhard Schroeder aitisha uchaguzi wa mapema
23 Mei 2005Kansela wa ujerumani Gerhard Schroeder ametaka kufanyike uchaguzi mkuu mapema kabla ilivyokuwa imepangwa.
Uamuzi wa Kansela umetokana na chama chake cha Social Demokrats kushindwa katika uchaguzi wa hapo jana wa jimbo la Noth Rhine Westphalia.
Jimbo hilo limekuwa ngome ya chama cha Social Demokrats kwa takriban miaka 40.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali Chama cha Christian Demokrats kinachongozwa na Angela Merkel kilijipatia asilimia 45 ya kura ikilinganishwa na asilimia 37 iliyojipatia chama cha bwana Schroeder.
Matokeo mabaya kwa upande wa chama cha bwana Scroeder wachunguzi wanasema yametokana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira hapa ujerumani na mageuzi ambayo hayakukubalika na wananchi.
Kiongozi wa chama cha cha CDU Angela Merkel ambaye huenda akapambana na bwana Schroeder katika uchaguzi ujaio katika juhudi zake za kuwa kansela wa kwanza mwanamke hapa ujerumani amesema wapiga kura wamekiamini chama hicho wakikitaka kuunda sera itakayopunguza ukosefu wa ajira hapa ujerumani. Bi Angela ameliunga mkono penmdekezo lilitolewa na Schoeder la uchaguzi wa mapema.
Kwa mujibu wa katiba ya Ujerumani uchaguzi unaweza kufanyika mapema iwapo rais atauitisha.Serikali pia lazima ishindwe katika kura ya kutokuwa na imani nayo bungeni.