1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela Merkel akamilisha ziara ya Bara Asia

1 Septemba 2007

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amerejea nyumbani kutoka ziara yake ya siku saba barani Asia.Ziarani nchini China na Japan,suala la ulinzi wa mazingira lilipewa kipaumbele katika majadiliano ya Kansela Merkel.Alipozungumza mjini Kyoto,ambapo ndipo mkataba wa Itifaki ya Kyoto kuhusu ulinzi wa mazingira ulitiwa saini miaka kumi iliyopita,Merkel alitoa mwito kwa mataifa yanayoinukia kiuchumi kuweka malengo yalio wazi kupambana na ongezeko la joto duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW