BERLIN: Kansela Merkel kuzungumza suala la Darfur
25 Agosti 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel atakuwa na majadiliano ya uhakiki pamoja na serikali ya Beijing wakati wa ziara yake nchini China.Katika hotuba yake ya kila juma kwenye mtandao wa Internet,Merkel amesema,anatazamia kujadili matatizo yanayohusika na haki za binadamu na bidhaa za China.
Akaongezea kuwa China ina uhusiano wa karibu na Afrika,kwa hivyo atajadiliana na viongozi wa China juu ya njia za kupambana na ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la Darfur nchini Sudan.China inatuhumiwa kuwa haijitahidi vya kutosha,kuzuia umwagaji damu katika Darfur.Ziara ya Kansela Merkel barani Asia,inayoanza siku ya Jumapili,itampeleka China na Japan.