1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Katiba ya umoja wa ulaya yaidhinishwa na Iran yapewa onyo.

13 Mei 2005

Bunge la kadri la shirikisho la Ujerumani Bundestag limeidhinisha mswada wa katiba ya umoja wa ulaya kwa kauli moja.

Mswaada huo ulipata wingi wa kura 569 huku kura 23 zikiupinga na kura mbili hazikupigwa.

Uamuzi huo unaifanya Ujerumani kuwa taifa kubwa zaidi kuunga mkono mswaada wa katiba ya umoja wa ulaya.

Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani vimesema vina imani kuwa mswaada huo utapita bila kupingwa pindi utakapo wasilishwa kupigiwa kura kwenye bunge kuu Bundestrat tarehe 27 mwezi huu siku mbili kabla Ufaransa kupiga kura ya maoni juu ya mswaada huu.

Wakati huo huo Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zimetuma barua kwa Iran kuionya juu ya matatizo yatakayotokea iwapo nchi hiyo inatarajia kuendelea na hatua yake ya kutaka kuanzisha tena mpango wake wa kinuklia.

Ilani hiyo imetolewa kufuatia mkutano baina ya Tehran na maafisa wa umoja wa ulaya pamoja na shirika la kimataifa la nguvu za atomiki.

Serikali ya Iran bado inashikilia kuwa mpango wake wa kinuklia hauhusiani kamwe na nia ya kutaka kutengeneza silaha za kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW