BERLIN : Kerkorian kununuwa Chryler kwa euro bilioni 3.3
6 Aprili 2007Matangazo
Kundi la uwekezaji la tajiri mkubwa wa Marekani Kirk Kerkorian linataka kuipatia kampuni ya kutengeneza magari ya Ujerumani na Marekani ya DaimlerChrysler euro bilioni 3.3 taslimu kununuwa kitengo chake cha Chrysler kinachozorota.
Shirika la Tracinda ambayo ni kampuni inayoshikilia mali za Kerkorian imethibitisha kuwepo kwa azma hiyo kwenye taarifa ya maandishi. Msemaji wa DaimlerChrysler amekataa kuzungumzia habari hizo.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya magari ya Ujerumani na Marekani Dieter Zetsche amethibitisha kwa mara ya kwanza hapo jana kwamba kampuni hiyo iko katika mazungumzo yenye lengo la kumtafuta mnunuzi wa Chrsyler na kwamba hatua zote zimewekwa wazi.