1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Ujerumani asema Ufaransa na Ujerumani zitabaki kuwa nguvu kuu za kuuendesha umoja wa Ulaya.

20 Julai 2005

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa ushirikiano kati ya Ujerumani na Ufaransa ni lazima ubaki kuwa nguvu kuu ya kuendesha umoja wa Ulaya.

Wakati wa ziara yake mjini Paris, Merkel ametaka kumhakikishia rais wa Ufaransa Jacques Chirac kuwa Ufaransa itabaki kuwa mshirika muhimu wa Ujerumani hata kama atachukua nafasi ya mshirika wake mkuu kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo Septemba.

Merkel pia alikutana na waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu Dominique de Villepin, ambao wote wanaonekana kuwa na uwezekano wa kuchukua nafasi ya Bwana Chirac wakati muda wake utakapomalizika hapo 2007.