BERLIN : Madereva wa treni waahirisha mgomo
11 Oktoba 2007Matangazo
Chama cha wafanyakazi madereva wa treni nchini Ujerumani GDL kimesema hakitoendelea na mgomo waliokuwa wametishia kufanya leo hii.
Mgomo huu yumkini ukaitishwa tena iwapo kampuni ya reli ya taifa Deutsche Bahn itashindwa kuidhinisha ongezeko la mishahara na masharti ya chama hicho cha wafanyakazi madereva wa treni.
Maelfu ya madereva wanaowakilishwa na chama hicho cha GDL walisita kufanya kazi kwa masaa kadhaa wakati wa saa za harakati Ijumaa iliopita na kitibuwa kwa kiasi kikubwa sana usafiri wa reli.