BERLIN : Madereva wa treni wamaliza mgomo wa masaa 62
17 Novemba 2007Matangazo
Madereva wa treni nchini Ujerumani wamerejea kazini kufuatia kumalizika mgomo mkubwa kabisa wa reli ulioikumba nchi.
Hata hivyo chama cha wafanyakazi madereva wa reli kimetishia kufanya mgomo zaidi wiki ijayo.Mgomo huo wa masaa 62 juu ya mzozo wa mishahara umeathiri usafiri wa mizigo kadhalika ule wa abiria.Mgomo huo umesitisha usafiri wa takriban asilimia 75 ya treni Ujerumani ya mashariki na asilimia 50 ya treni magharibi mwa Ujerumani.
Baadhi ya kampuni ikiwemo ile ya kutengeneza magari ya Audi zimelazimika kufuta shifti za kazi kutokana na ukosefu wa vipuri na makontena ya kusafirishia mizigo kulimbikana kwenye bandari kubwa kabisa nchini Ujerumani ya Hamburg.