BERLIN : Mageuzi ya afya yavuka kikwazo cha mwisho
17 Februari 2007Matangazo
Mpango wa mageuzi ya mfumo wa huduma za afya wa eerikali ya mseto ya Ujerumani umevuka kikwazo cha mwisho cha kisheria baada ya kupitishwa na bunge la Ujerumani Bundesrat.
Kansela Angela Merkel amesema mageuzi hayo yatapunguza gharama na urasimu katika mifumo yote miwili ya huduma za afya wa taifa na ule wa binafsi.
Wanaokosa mageuzi hayo wanasema mpango wa mabadiliko hayo uliofikiwa kati ya chama cha kihafidhina cha Merkel cha Christian Demokrat na kile cha Social Demokrat utazidisha urasimu na kuongeza gharama kwa watumiaji ambao hulipia mifumo hiyo.