1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Maonyesho ya utalii ITB

12 Machi 2005

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameyafungua mjini Berlin maonyesho makubwa kabisa ya utalii duniani,akitoa wito kwa wasafiri kurejea kwenye pwani za nchi za Asia zilizoathirika kwa Tsunami.Schroeder amesema utalii ni njia muhimu kabisa ya kutoa msaada wa kimataifa kwa nchi za Bahari ya Hindi ambazo ziliteketezwa kwa mafuriko ya Tsunami Desemba 26.Suala kuu litakalojadiliwa katika maonyesho ya utalii mjini Berlin,ni njia ya kufufua utalii na imani ya wasafiri kwenda katika yale maeneo yalioathirika kwa Tsunami.Kiasi ya wageni 140,000 wanatazamiwa kuyatembelea maonyesho ya Berlin ambako zaidi ya makampuni 10,000 kutoka nchi 180 yanashiriki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW