Berlin. Marekani yaongeza ulinzi katika ubalozi wake.
21 Aprili 2007Matangazo
Marekani imeongeza ulinzi katika ubalozi wake nchini Ujerumani kutokana na kile maafisa wanachosema kuwa ni kitisho kikubwa.
Msemaji wa ubalozi huo wa Marekani mjini Berlin amesema kuwa hatua hiyo inafuatia tahadhari kutoka kwa maafisa wa Ujerumani kuwa nchi hiyo inakabiliwa na kitisho cha shambulio la kigaidi kutokana na kujiingiza kwake zaidi kijeshi nchini Afghanistan.
Raia wa Marekani nchini Ujerumani wameshauriwa kujichunga.