BERLIN: Mateka wa Kijerumani aliuawa kwa risasi
3 Agosti 2007Matangazo
Mhandisi wa Kijerumani aliefariki alipokuwa amezuiliwa mateka nchini Afghanistan,aliuawa kwa risasi na wateka nyara wake.Habari hiyo imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani mjini Berlin,baada ya maiti ya mateka huyo kufanyiwa uchunguzi mjini Cologne baada ya kurejeshwa Ujerumani juma lililopita.Mjerumani mwengine aliekamatwa wakati mmoja na marehemu,bado amezuiliwa na wateka nyara nchini Afghanistan. Juhudi za kupata uhuru wa mateka huyo wa Kijerumani zinaendelea.
Waziri wa Dola katika Wizara ya Nje ya Ujerumani,Gernot Erler amesema,serikali hailezi njia zinazotumiwa kuokoa maisha ya mateka huyo.Wanafanya kinachowezekana kibinadamu lakini pia kinachowajibika na sio kitakachowatia moyo wahalifu wengine kuigiza kitendo cha aina hiyo.