1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mazungumzo ya wazi kati ya serikali na Waislamu

26 Septemba 2006

Waziri wa serikali ya shirikisho ya Jamhuri ya Ujerumani akiwa katika harakati wiki hii za kuwajumuisha Waislamu kwenye jamii ya kawaida ya Ujerumani hapo jana ametowa wito wa kufanyika kwa mazungumzo kinaga ubaga na viongozi 15 waliochaguliwa kuwawakilisha Waislamu nchini.

Mkutano wa Uislamu uliopangwa kufanyika hapo kesho unatarajiwa kuanzisha mazungumzo yatakayodumu kwa miaka miwili hadi mitatu yenye nia ya kuanzisha masomo ya Kiislam katika shule za Kijerumani pamoja na kuwashawishi Waislamu wazikubali asasi za Kijerumani.

Waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schaeuble amesema Uislamu hivi sasa ni sehemu ya Ujerumani na kwamba mkutano huo unapaswa uwe wazi juu ya matatizo wanayoyakabili.

Amesema katika mahojiano yatakayochapishwa leo hii na gazeti la kila siku la Suedeutsche Zeitung kwamba hawatoanza mazungumzo hayo kwa maneno ya kirafiki na kwamba Uislamu lazima ukubali kanuni za msingi na maadili ambayo yanaunda Ujerumani na Ulaya.