Berlin. Merkel arejea kutoka Afrika.
8 Oktoba 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili mjini Berlin akitokea katika ziara yake ya kwanza ya mataifa matatu ya Afrika. Katika kituo chake cha mwisho cha ziara yake hiyo alifanya mazungumzo na rais wa Liberia Ellen Johnson –Sirleaf , rais wa kwanza mwanamke nchini humo. Merkel amesema ziara yake hiyo ilikuwa na lengo la kutoa ishara ya kumuunga mkono Sirleaf, ambaye anakabiliwa na jukumu zito la kuujenga uchumi wa Liberia baada ya miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Serikali ya Ujerumani imesema itaongeza msaada wake wa maendeleo kwa Liberia na kuongeza juhudi za kutaka madeni ya nchi hiyo yafutwe.