BERLIN: Mhandisi wa Kijerumani yungali mateka
5 Agosti 2007Matangazo
Licha ya kufanywa majadiliano ya bidii,hakuna maendeleo yaliyopatikana kuhusu mateka waliozuiliwa na Taliban nchini Afghanistan. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani mjini Berlin,amearifu kuwa kamati ya dharura inaendelea na juhudi za kupata uhuru wa mhandisi wa Kijerumani alietekwa nyara Afghanistan.