BERLIN: Mkutano kati ya serikali na wajumbe wa waislamu
27 Septemba 2006Matangazo
Wajumbe 15 wa jumuiya ya waislamu wanaoishi Ujerumani,hii leo wanakutana na maafisa wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin.Azma ya mkutano huo ni kuanzisha kile kinachotarajiwa kuwa majadiliano ya miaka miwili hadi mitatu kati ya serikali na waislamu.Waziri wa ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble anauongoza mkutano huo katika kasri la Charlottenburg mjini Berlin. Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni hali ya wanawake katika uislamu,maingiliano kati ya serikali na dini na masomo ya dini ya kiislamu katika shule za Ujerumani.