1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mkutano wa serikali na Waislamu waanza leo

27 Septemba 2006

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani leo ataongoza mkutano wa viongozi kati ya maafisa wa serikali na viongozi wa Waislamu nchini na kuanzisha kile kinachotarajiwa kuwa mdahalo wa miaka miwili juu ya namna ya kuwajumuisha kwa njia bora zaidi katika jamii ya Kijerumani Waislamu zaidi ya milioni tatu walioko nchini.

Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na mtafuruku uliozushwa kutokana na mchezo wa tamthiliya uliotungwa na kundi mashuhuri la Mozart la Berlin kufuta sehemu ya igizo lake lenye kuonyesha vichwa vilivyokatwa vya Yesu, Buddha na Muhammad kutokana na wasi wasi wa kiusalama.

Waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schaeuble ambaye ametupilia mbali uamuzi wa kundi hilo kuondowa sehemu ya igizo hilo kuwa ni wendawazimu amesema kwamba mazungumzo na viongozi wa Kiislam mjini Berlin yatakuwa wazi kwa kuwa Uislamu ni sehemu muhimu ya Ujerumani na Ulaya kwa hiyo lazima pia ukubali kanuni na maadili yanayounda Ulaya.

Afisa mwandamizi wa usalama amesema itawekwa wazi kwenye mkutano huo kwamba katiba na kanuni zake za kisheria havina mjadala.