BERLIN : Mkuu wa Siemens yuko katika shinikizo
22 Aprili 2007Uchunguzi juu ya madai ya rushwa katika kampuni kubwa kabisa ya vifaa vya elektronik nchini Ujerumani Siemes umepelekea kutolewa kwa wito kwa mkuu wa ushauri wa bodi yake Heinrich van Pierer pia kusitisha dhima yake ya kuwa mshauri kwa serikali.
Pierer anbaye ni mwenyekiti wa baraza la ubunifu la Kansela Angela Merkel amesema hapo Alhamisi atan’gatuka katika bodi ya Siemens lakini amekanusha kuwa na makosa.
Wabunge waandamizi wa chama cha Social Demokrat kilioko kwenye serikali ya mseto nchini Ujerumani na wapinzani wa Kiliberali wametowa wito huo lakini Thomas Steg msemaji wa Merkel amesema Kansela huyo anataka Pierer aendelee kubakia kama mshauri wa serikali.Kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa kampuni ya IG Metal katika mkoa wa Bavaria Werner Neugebauer amedai kwamba Pierer alikuwa akijuwa juu malipo yanayodaiwa kufanywa kwa chama hasimu kidogo cha wafanyakazi.
Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Siemens ilitumia fungu la fedha kwa ajili ya kuhonga ili kupatiwa kondarasi za kigeni.