BERLIN: Mradi wa nyuklia wakosolewa na Ujerumani
28 Julai 2007Matangazo
Wanasiasa nchini Ujerumani wamekosoa mpango wa Ufaransa wa kutaka kujenga kinu cha nyuklia nchini Libya.Mwenyekiti-mwenza wa chama cha upinzani cha Kijani nchini Ujerumani,Reinhard Bütikofer ameueleza mpango huo kama ni „harakati hatari za kizalendo.“
Wanasiasa wengine kutoka vyama CDU na SPD vya serikali ya mseto ya Ujerumani wamesema,hatua ya Ufaransa inachukuliwa mapema mno na huenda ukawa hatari.
Siku ya Alkhamisi,Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy alitia saini taarifa ya maelewano pamoja na Libya,ikihusika na makubaliano ya kujenga kinu cha nishati ya nyuklia.