BERLIN : Muafaka kwa mageuzi ya huduma za afya
13 Januari 2007Waziri wa Afya wa Ujerumani amesema umefikiwa muafaka wa mwisho juu ya mipango ya kuufanyia mageuzi mfumo wa huduma za afya nchini wa euro bilioni 140.
Waziri wa Afya Ulla Schmidt ameulezea muafaka huo uliofikiwa na vyama mbali mbali kuwa ni ushindi.Amesema rasimu ya sheria hiyo iliofanyiwa marekebisho itaweza kufikishwa bungeni ili kuidhinishwa hivi karibuni ina inatazamiwa kuanza kazi tarehe Mosi mwezi wa April.
Mpango huo wa mageuzi ya huduma za afya unakusudia kupunguza gharama kubwa za mfumo wa huduma za afya nchini Ujerumani na kuufanya uwe wa wazi kwa wafanyakazi wanaougharimia kwa kupitia michango ya lazima.
Wanaoukosowa mpango huo mpya wanasema mabadiliko hayo hayotosaidia sana kutatuwa tatizo la muda mrefu la kuwaondolea mzigo wa michango wafanyakazi.