BERLIN : Mwaka mmoja zaidi operesheni dhidi ya ugaidi
15 Novemba 2007Matangazo
Bunge la Ujerumani leo hii limepiga kura kuongeza muda wa kushiriki kwa jeshi la Ujerumani katika shughuli za kupambana na ugaidi katika Operesheni Dumisha Uhuru nchini Afghanistan.
Vyama vya Christian Demokratik,Social Demokratik na kile cha Kiliberali vyote vimepiga kura kuunga mkono kuongeza muda huo kwa mwaka mmoja zaidi.Hivi sasa kuna wanajeshi wa Ujerumani 1,400 nchini Afghanistan.
Chama cha Left cha mrengo wa shoto la kile cha Kijani viluikuwa vinapinga kuendelea kushiriki zaidi kwa jeshi hilo vikisema kwamba bado hakuna mamlaka ya Umoja wa Mataifa kwa shughuli hiyo ambayo ilianza kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 nchini Marekani.