1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Peres aisifu Ujerumani kwa kutuma wanamaji kulinda pwani ya Lebanon

5 Oktoba 2006

Makamu waziri mkuu wa Israel, Shimon Peres, ameisifu Ujerumani kwa kutuma meli za jeshi la wanamaji kulinda usalama katika pwani ya Lebanon.

Akizungumza wakati wa ziara yake rasmi mjini Berlin, Perez aliwaambia waandishi habari kuwepo kwa wanamaji wa Ujerumani katika pwani ya Lebanon kutasaidia kupunguza idadi ya silaha zinapolekewa wanamgambo wa Hezbollah.

Wakati huo huo, meli nane za kwanza za Ujerumani zikiwa na wanajeshi takriban 1,000 zilitia nanga katika bandari ya Cyprus hapo jana. Ukaguzi wa awali katika pwani ya Lebanon umepangwa kuanza hii leo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW