BERLIN: Rais Köhler amekataa kumsamehe Klar
8 Mei 2007Matangazo
Christian Klar,mpiganaji wa zamani wa kundi la kigaidi la Jeshi Jekundu-(RAF) kwa hivi sasa, ataendelea kubakia jela.Siku ya Jumatatu,taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais Horst Köhler wa Ujerumani imesema,Köhler amekataa kumsamehe mpiganaji huyo wa zamani wa RAF.Kwa hivyo, Klar mwenye umri wa miaka 54 aliekaa jela tangu miaka 24 atabakia jela angalao hadi mwaka 2009. Klar anatumikia kifungo cha maisha kwa kuhusika na mauaji mbali mbali yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Jeshi Jekundu.Baadhi ya viongozi wa kihafidhina katika serikali ya Kansela Angela Merkel walimkosoa rais Köhler kwa kukutana na Klar kabla ya kupitisha uamuzi wake.