BERLIN: Rais wa shirikisho la Ujerumani Horst Köhler asisitiza ajira kwa wananchi.
16 Machi 2005Matangazo
Rais wa shirikisho la jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler ameihimiza serikali na upande wa upinzani wazidishe juhudi za pamoja kupambana na ukosefu wa ajira uliokithiri hapoa Ujerumani ambapo zaidi wa watu milioni tano na laki mbili hawana ajira.
Katika hotuba yake kuhusu mageuzi aliyoitoa mbele ya wawakilishi wa kiuchumi na kijamii mjini Berlin rais wa shirikisho Horst Köhler ametaja baadhi ya hatua zitakazo saidia kubuni n afasi za kazi kuwa ni pamoja na mageuzi katika mfumo wa kodi ya mapato, kupunguzwa marupurupu ya fedha yanayotolewa na waajiri.
Hotuba hiyo ya rais wa shirikisho la Ujerumani Horst Köhler imesifiwa na pande zote.