BERLIN : Rais wa Ujerumani alikuwa akipelelezwa
25 Novemba 2006Matangazo
Gazeti la Ujerumani la Der Spiegel limeripoti kwamba Wizara ya Usalama ya Ujerumani Mashariki Stasi kwa miaka mingi imekuwa ikimpeleleza Rais wa sasa wa Ujerumani Horst Köhler.
Kupelelezwa huko kwa Kohler kumefanyika wakati akiwa muajiriwa wa wizara ya fedha.
Rais huyo amesema amekuwa akifahamu juu ya kufichuliwa kwa taarifa hizo za ujasusi kwa wiki kadhaa sasa na tayari ameliangalia jalada lake la Stasi.