1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN Schröder akanusha mpango wa kutaka kujiuzulu

8 Juni 2005

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder ameipuuza ripoti iliyotolewa na chombo kimoja cha habari humu nchini kikisema kwamba chama chake cha SPD kina mpango wa kumtaka yeye ajiuzulu, badala ya kugombea wadhifa wake katika kinyang´anyiro kijacho cha uchaguzi, ambao yuko tayari kushindwa.

Inasemekana chama hicho kinamtaka mwenyekiti wake, Franz Münterfering, kuichukua nafasi ya Schröder, ili muungano wa chama cha SPD na chama cha Kijani uendelee kubakia madarakani hadi uchaguzi wa mwaka wa 2006.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW