BERLIN :Schroeder aiomba radhi Russia kwa maafa ya vita
8 Mei 2005Matangazo
Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameomba radhi kwa Russia kwa maafa makubwa na hasara waliyopata wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Schroeder amekiri kwamba wananchi wa Russia waliteseka kutokana na vita hivyo vya Manazi wa Ujerumani na kwa hiyo amewataka wawasamehe.
Kuomba radhi huko kwa kiongozi huyo wa Ujerumani kumechapishwa katika gazeti la Russia la Komsomol Pravda.Amesema anauona mwaliko wa Rais Vladimir Putin wa Russia kushiriki katika kubukumbu ya hapo kesho mjini Moscow ya miaka 60 ya kumalizika kwa vita hivyo kuwa ni ushahidi wa uaminifu kwa wananchi wa Ujerumani.