1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Schroeder akaribisha mazungumzo ya Marekani na Ulaya

20 Februari 2005

Kansela Gerhrad Schroeder wa Ujerumani ameikaribisha kauli iliyotolewa na Rais George W Bush wa Marekani ya kutaka kuwepo kwa mazungumzo ya kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Ulaya.

Bush na Schroeder wanatarajiwa kuwa na mazungumzo mjini Mainz nchini Ujerumani hapo Jumaatano.Mapema Bush amesema atakukaribisha kushiriki zaidi kwa Ujerumani katika kuijenga upya Iraq.Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Ujerumani cha ARD Bush amesema kwamba msaada wa Ujerumani utathaminiwa sana katika kulijena upya taifa la Iraq na kutowa misaada ya kibinaadamu kama vile inavyofanya nchini Afghanistan.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo ya Rais Bush Barani Ulaya ambayo inaanza rasmi leo hii miji kama vile wa Brussels nchini Ubelgiji imekuwa ikichukuwa tahadhari kwa kuimarisha usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW