1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Schroeder asema kutanuka kwa Umoja wa Ulaya ni mafanikio

1 Mei 2005

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amesema anaamini kwamba kutanuka kwa Umoja wa Ulaya mwaka jana hadi kuwa na mataifa wanachama 25 kumemnufaisha kila mtu.

Nchi 10 wanachama wapya nyingi zikitoka iliyokuwa Urusi ya zamani zimejiunga na umoja huo hapo tarehe Mosi Mei mwaka mmoja uliopita.Kauli hiyo ya Schroeder imeungwa mkono na Rais Horst Köhler wa Ujerumani ambaye amezinduwa kuanza kwa mwaka wa Ujerumani na Poland hapo jana.Köhler ambaye aliungana na Rais mwenzake wa Poland Aleksander Kwasnieswki mjini Berlin amesema kujiunga kwa Poland katika umoja huo hapo mwaka 2004 kumetowa nafasi ya kuimarishwa kwa uchumi wa nchi zote mbili Ujerumani na Poland.

Mwaka wa Ujerumani na Poland ni mfululizo wa matukio ya kitamaduni zaidi ya 1,000 ambayo yatafanyika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW