BERLIN : Serikali haikuzuwiya kuachiliwa Kurnaz
30 Machi 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amekanusha shutuma kwamba serikali ya Ujerumani ilikataa pendekezo la Marekani kumuachilia huru mwanaume wa Kituruki mzalia wa Ujerumani kutoka kambi ya gereza la Marekani huko Guntanamo Bay hapo mwaka 2002.
Steinmeir ambaye wakati huo alikuwa katibu mwandamizi wa Kansela wa zamani Gerhard Schroeder ameiambia kamati ya bunge kwamba Ujerumani haikurefusha kwa njia yoyote ile muda wa kushikiliwa kwa Murat Kurnaz.
Ushahidi wake huo unafuatia ushahidi kama huo uliotolewa na waziri wa mambo ya ndani wa zamani wa Ujerumani Otto Schily mapema hapo jana.
Kurnaz ambaye alikamatwa kama mtuhumiwa wa ugaidi nchini Pakistan hapo mwaka 2001 aliachiliwa huru kutoka Guantanamo mwaka jana.