BERLIN: Serikali ya Ujrumani yaidhinisha mabadiliko ya mfumo wa afya
25 Oktoba 2006Matangazo
Baraza la mawaziri la Ujerumani limeidhinisha mabadiliko ya mfumo wa afya ambayo yamesababisha mpasuko katika serikali ya muungano ya kansela Angela Merkel.
Waziri wa afya Ulla Schmidt, amewaambia waandishi wa habari kwamba mswada huo wa sheria utasomwa bungeni kwa mara ya kwanza kesho kutwa Ijumaa na huenda ufanyike kuwa sheria ifikapo Aprili mosi mwaka ujao.
Mswada huo ni matokeo ya mjadala mkali ambao umekuwa ukiendelea kati ya chama cha Christian Democrats na chama cha Social Democrats. Mabadiliko hayo yanalenga kuongeza fedha kwa mfumo wa afya.
Wataalamu wameonya kwamba mswada huo hauwezi kukabiliana na idadi ya wananchi wanaoendelea kuzeeka na gharama za huduma za matibabu zinazoendelea kuongezeka.