BERLIN-SPD na cahama cha Kijani kufanya kampeni tofauti kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba.
25 Mei 2005Vyama vya SPD na cha Kijani vilivyomo katika serikali ya muungano ya Ujerumani,vimesema vitafanya kampeni zake tofauti katika uchaguzi mkuu wa taifa unaokuja.
Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder ameliambia gazeti litolewalo kila wiki la Die Zait,kuwa anafikiria kushirikiana na ama na chama cha Kijani au kile cha upinzani cha wahafidhina cha CDU.Matamshi hayo yamekuja kufuatia tangazo lake la ghafla la kufanyika uchaguzi wa mapema tarehe 18 mwezi wa Septemba,ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya muda wake.
Kansela Schröder amesema atawasilisha muswada wa kura ya imani Bungeni itakapofika tarehe mosi mwezi wa Julai,kura ambayo hatma yake itakuwa kuvunjwa kwa Bunge.
Chama chake cha Social Democrats kilishindwa vibaya na chama cha CDU katika uchaguzi uliofanyika Jumapili katika mkoa wa North Rhine-Westphalia.
CDU kimedokeza kuwa kiongozi wake Angela Merkel,ndie atakuwa mgombea wao katika uchaguzi huo wa mwezi Septemba.