1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Steinmeier aonya dhidi ya kuivamia Iran

28 Oktoba 2007

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ameonya dhidi ya kuivamia kijeshi Iran kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia.

Waziri Steinmeir ametoa onyo hilo kwenye mkutano wa chama cha Social Democratic, SPD, mjini Hamburg huku wasiwasi ukizidi kuongezeka kwamba Marekani inapania kuivamia Iran.

Frank Walter Steinmeir amesema kila jitihada zinatakiwa kufanywa ili kuzuia silaha za kinyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati, lakini akasisitiza kwamba Ujerumani lazima iendelee kutafuta suluhisho la kidiplomasia pamoja na Marekani, Urusi na China.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW