BERLIN: Stoiber apinga kupeleka wanajeshi zaidi wa Kijerumani
18 Agosti 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa jimbo la Bayer kusini mwa Ujerumani,Edmund Stoiber anapinga kupeleka wanajeshi zaidi wa Kijerumani nchini Afghanistan. Amesema,ikiwa vikosi vya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO,vinahitaji kuimarishwa basi kwanza ni mataifa mengine yanayowajibika kwani Ujerumani tayari inatoa mchango mkubwa.