1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Uamuzi wa chama cha Kijani wakosolewa

16 Septemba 2007

Nchini Ujerumani,uamuzi wa chama cha Kijani kupinga kurefusha ujumbe wa kijeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan,unazidi kukosolewa.Katibu Mkuu wa chama cha CDU,Ronald Pofalla amesema, yadhihirika kuwa chama cha Kijani hakitaki kuwajibika kwa niaba ya umma wa Afghanistan.

Siku ya Jumamosi,wanachama wa Kijani katika mkutano maalum ulioitishwa mjini Göttingen, walikwenda kinyume na viongozi wa chama hicho na walitoa mwito kwa wabunge wao kupinga ujumbe wa ndege za upelelezi za Ujerumani,aina ya Tornado zinazosaidia vikosi vya amani vya kimataifa, nchini Afghanistan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW