BERLIN: Uanachama wa Poland katika Umoja wa Ulaya umeleta mafanikio
1 Mei 2005Matangazo
Rais wa Ujerumani Horst Köhler na rais Aleksander Kwasniewski wa Poland wamehudhuria sherehe ya kuadhimishwa mwanzo wa mwaka wa „Ujerumani na Poland“.Kutakauwepo zaidi ya matukio 1,000 ya kitamaduni katika kipindi cha miezi 12 ijayo.Rais Köhler katika hotuba yake amesema,uanachama wa Poland katika Umoja wa Ulaya mwaka mmoja uliopita,umesaidia kuimarisha uchumi wa Poland na Ujerumani.