1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ufaransa na Ujerumani wazungumzia masuala nyeti

7 Machi 2005

Ufaransa na Ujerumani zimehakikisha tena uhusiano wao wa kirafiki. Wakizungumza na waandishi habari Baada ya mkutano wao Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder na rais wa Ufaransa Jacque Chirac wamesema wamekubaliana kuhusu masuala kadha ya yanayohusu masuala nyeti ya Umoja wa ulaya pamoja na masuala ya kimataifa.

Viongozi hao wawili pia wametaka kuwepo mageuzi ya mfumo mzima wa kuimarisha sarafu ya Ulaya na ukuaji uchumi dhidi ya nchi zao.Ufaransa na Ujerumani zimelaumu mkataba wa kudhibiti bajeti za nchi za Umoja wa Ulaya ambapo unawajibisha nchi hizo kutovuka asilimia tatu ya pato jumla la taifa,katika nakisi za bajeti zao.