Berlin. Ujerumani haitasalimu amri kwa wateka nyara.
13 Aprili 2007Matangazo
Ofisi ya wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani imesema kuwa kikosi cha kutanzua mizozo kinaendelea kufanyakazi ili kuweza kupata kuachiwa huru kwa mwanamke mmoja Mjerumani pamoja na mwanae wa kiume ambao walikamatwa nchini Iraq miezi miwili iliyopita.
Msemaji wa serikali mjini Berlin amesisitiza kuwa kukubali madai ya wateka nyara ni suala ambalo halipo.
Wapiganaji wametishia kumuua mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 61 Hannelore Krause na mwanae mwenye umri wa miaka 20 Sinan, hadi pale Ujerumani itakapoanza kuondoa majeshi yake kutoka Afghanistan katika muda ambao umekwisha pita.
Hakuna taarifa mpya zilizotolewa juu ya hali ya mzozo huo.