1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani imeamua kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Kosovo na Afghanistan.

25 Juni 2005

Waziri wa mambo ya ndani nchini Ujerumani Bwana Otto Schilly na wenzake kutoka majimbo 16 ya nchi hiyo wamekubaliana kuwa wakimbizi ambao waliingia nchini Ujerumani wakati wa machafuko yaliyotokea huko Kosovo na Afghanistan sasa watapaswa kurejea nyumbani.

Haya ni matokeo katika mkutano uliofanyika mjini Stuttgart.

Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Baden-Württemberg , Heribert Rech amewaambia waandishi wa habari kufuatia mazungumzo yao kwamba hali katika nchi zote hizo mbili sasa ni swari na salama kwa wakimbizi hao kurejea.

Lakini amesema watu ambao hawajaoa watakabiliwa na hatua ya kuwarejesha Kosovo ama Afghanistan. Mawaziri hao pia wamekubaliana kuwa na sheria ngumu zaidi kwa ajili ya wahamiaji wa Kiyahudi kutoka Ulaya ya mashariki. Hivi sasa watahitajika kuonesha uwezo wao wa kuongea Kijerumani na wathibitishe kwamba ni wafuasi halisi wa imani ya dini ya Kiyahudi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW