1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani kuwapeleka wanajeshi Lebanon

27 Julai 2006

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amefanya mkutano na kamati ya maswala ya mambo ya kigeni kujadili uwezekano wa Ujerumani kuwapeleka wanajeshi wake nchini Lebanon.

Amesema mkutano uliofanyika jana mjini Roma Italia ni hatua muhimu ya kuutanzua mzozo huo na inaonyesha vipi wanasiasa wa kimataifa walivyofaulu kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali.

Steinmeier amepuuza madai kwamba mkutano huo ulishindwa kuvimaliza vita kati ya Israel na Hezbollah. Amesema, ´Mjadala uliokuwa mzuri na wa maana kubwa ni ikiwa jeshi la kimataifa la kulinda amani litafaulu kuleta utulivu na usalama zaidi katika eneo la mpakani kati ya Israel na Lebanon.´

Kamati ya bunge inakubali wanajeshi wa Ujerumani wapelekwe Lebanon lakini haijakubaliana juu ya kuitisha usitishwaji wa mapigano.

Vyama vya upinzani nchini Ujerumani vinailaumu serikali kwa kufanya machache kumaliza vita nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW