1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani na Israel zataka Iran izuiwe kupata silaha za kinuklia.

13 Desemba 2006

Ujerumani na Israel zimeitaka jumuiya ya kimataifa kutumia nafasi ya kidiplomasia , ikiwa ni pamoja na vikwazo , kuizuwia Iran kupata silaha za kinuklia.

Mjini Berlin , waziri mkuu anayefanya ziara nchini Ujerumani , Ehud Olmert na kansela wa Ujerumani Angela Merkel , pia wameshutumu mkutano unaokana kutokea mauaji ya halaiki ya Holokaust yaliyofanywa na Wanazi wa Ujerumani , mkutano unaofanyika nchini Iran na kuhudhuriwa na wanahistoria wanaotaka kuangalia upya historia.

Kuhusiana na nia ya Iran ya kujipatia teknolojia ya kinuklia , Merkel amesema muda umefika kwa vikwazo kutumika baada ya miezi kadha ya mvutano miongoni mwa mataifa makubwa kuhusiana na vipengee vya muswada wa azimio la umoja wa mataifa. Olmert amerudia msimamo wa Israel wa kutokukubali ama kukataa kuwa na silaha za kinuklia. Siku ya Jumatatu alizusha mshangao kwa kuelekea kuitaja Israel kuwa miongoni mwa nchi zinazomiliki silaha za kinuklia katika mahojiano. Mjini Berlin jana amesema kuwa matamshi hayo yamechukuliwa vibaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW