1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani yasifiwa kwa kutuma meli za doria Lebanon.

5 Oktoba 2006

Naibu waziri mkuu wa Israel Shimon Peres ameisifu Ujerumani kwa kutuma meli zake za kijeshi kufanya doria katika pwani ya Lebanon.

Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Berlin, amewaambia waandishi wa habari kuwa kuwapo kwa meli hizo katika mwambao wa Lebanon kunapunguza uingizaji silaha kinyume na sheria kwa wapiganaji wa Hizboullah.

Wakati huo huo , meli za kwanza nane za jeshi la Ujerumani zikiwa na karibu wanajeshi 1,000 zimetia nanga katika bandari ya Cyprus jana Jumatano.

Ujumbe wa kwanza wa doria katika pwani ya Lebanon utaanza leo Alhamis.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW