1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN Ujerumani yautaka umoja wa mataifa kuisadia tume ya kulinda amani kusini mwa Sudan

8 Juni 2005

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani bwana Peter Struck, atafanya ziara rasmi mjini New York, Marekani, mwezi huu kumhimiza katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan kuyatatua matatizo yanayoikabili tume ya kulinda amani kusini mwa Sudan, ambako Ujerumani inajukumu kubwa.

Struck amesema ana wasiwasi juu ya tume hiyo kuweza kusimamia amani kati ya serikali ya Sudan na waasi wa kusini wa Sudan´s Peoples Liberation Movement. Ameongeza kusema kwamba serikali ya Sudan ambayo pia inakabiliwa na mzozo mwengine mkubwa katika eneo la Darfur, haionyeshi ishara yoyote ya kuwakubali wapatanishi wa kimataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW