BERLIN : Ujerumani yumkini kutuma wanajeshi Lebanon
15 Agosti 2006Matangazo
Serikali ya Ujerumani inaonekana kukaribia kuidhinisha wanajeshi wa Ujerumani Bundeswehr kushiriki katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon.
Mdahalo sasa umehamia juu ya dhima itakayokuwa na kikosi hicho badala ya iwapo kitatumwa.Masuala ya kujadiliwa ni pamoja na kupeleka kikosi cha wanamaji kupiga doria katika mwambao nje ya bahari ya Lebanon na Israel,kutowa msaada wa kiufundi na kujenga upya miundo mbinu nchini Lebanon.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir yuko Mashariki ya Kati kuwatembelea viongozi nchini Jordan,Syria na Saudi Arabia kujadili hatua za kuchukuliwa baada ya kipindi cha vita.