1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Berlin: Urusi lazima impe Navalny huduma ya matibabu

13 Januari 2023

Ujerumani imeitaka Urusi kumpa huduma ya haraka ya matibabu mkosoaji wa Kremlin aliyeko gerezani, Alexei Navalny. Navalny amekuwa akilalamika kunyimwa ruhusa na maafisa wa gereza nchini Urusi kwenda kutibiwa hospitalini.

Alexei Navalny | russischer Oppositioneller
Picha: Pavel Golovkin/AP Photo/picture alliance

Ujerumani imeitaka Urusi kumpa huduma ya haraka ya matibabu mkosoaji wa Kremlin aliyeko gerezani, Alexei Navalny. Navalny amekuwa akilalamika kwa kunyimwa ruhusa na maafisa wa gereza nchini Urusi kwenda kutibiwa hospitalini.  Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Christiane Hoffmann, amesema Navalny anahitaji msaada wa dharura wa matibabu kama walivyosema madaktari kadhaa wa Urusi.

Berlin pia imesisitiza wito wa kutaka Navalny aachiliwe huru, ikisema kufungwa kwake jela kunatokana na kile inachokiita "hukumu iliyochochewa kisiasa". Mpinzani huyo maarufu wa Rais wa Urusi Vladmir Putin, alisema Jumatano kuwa ana dalili za mafua ikiwemo homa lakini anazuliwa katika chumba cha adhabu katika gereza lenye ulinzi mkali nje ya mji mkuu Moscow na kunyimwa matibabu ya msingi.