BERLIN: Ushirikiano wa kiuchumi na sayansi kuimarishwa zaidi
27 Oktoba 2007Matangazo
Ujerumani inataka kushirikiana zaidi na India katika sekta za uchumi na sayansi.Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema,biashara ya zaidi ya Euro bilioni 10 inayofanywa kati ya nchi hizo mbili ni motisha.
Siku ya Jumatatu,Kansela Merkel anaanza ziara yake rasmi nchini India,akifuatana na tume kubwa ya wachumi na waziri wa utafiti,Annette Schavan.